Head image
Govt. Logo

Hits 100424 |  4 online

           


RIPOTI YA KAMATI YA KUSIMAMIA OFISI ZA VIONGOZI WAKUU WA KITAIFA KWA OFISI YA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS, ZANZIBAR.
news phpto

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe Harusi Said Suleiman akiwasilisha Ripoti ya Utekelezaji wa Maoni, Ushauri na Mapendekezo yaliyotolewa na Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa kwa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais. Kwenye Baraza la 10 la Wawakilishi Zanzibar, mkutano wa 12.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe Harusi Said Suleiman amesema Ofisi yake imepokea miongozo na maelekezo yaliyotolewa na Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa kwa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais na kuahidi kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa faida ya wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.

Mhe Harusi ameyasema hayo wakati akiwasilisha ripoti ya utekelezaji wa maoni, ushauri mapendekezo yaliyotolewa na Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa kwa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais mwaka 2022 – 2023, kwenye Baraza la 10 la Wawakilishi Zanzibar, mkutano wa 12.

Waziri Harusi amesema ushauri na mapendekezo yaliyotolewa yana dhamira ya kuhakikisha kwa kunakuwepo utekelezaji wenye ufanisi unaoleta tija kwa jamii ambapo jumla ya hoja 17 zilitolewa na kuelekezwa kwenye taasisi za Mazingira, Tume ya UKIMWI na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya.

Akisoma ripoti ya Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa Mhe Abdalla Abasi Wadi kwa niaba ya mwenyekiti wa Kamati hio Mhe Machano Othman Said amesema kuwa kamati imetekeleza wajibu wake wa kujadili ipasavyo na kuhoji mambo mbali mbali ambayo yametolewa ufafanuzi.

Aidha, kamati inaiyomba jamii kuunga mkono juhudi za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya, mapambano dhidi ya gonjwa la UKIMWI pamoja na kuiasa jamii kutojishirikisha na vitendo vyote viovu ambavyo vinaharibu haiba, mila na silka ya wazanzibari.

Uwasilishaji wa ripoti unafuatia Kanuni ya 107(3) ya Kanuni za Baraza la Wawakilishi Zanzibar, toleo la 2020 ambapo Kamati zimepewa jukumu la kufuatilia utekelezaji wa maoni na ushauri wa kamati yaliyotolewa katika Ripoti ya Kamati ya mwaka uliotangulia.

Huduma za Tehama

Barua Pepe

Sisi

Mwanzo Kuhusu Sisi Idara Zetu

Viunga Muhimu

ZEMA ZAC DDA IKULU

Mawasiliano

Ofisi Kuu
S.L.P 2808, Migombani, Zanzibar
Tel.: +255(24)2232474 Mhe WaziriTel.: +255 (24)2232475 Katibu Mkuu,
Fax: +255 (24)2232476
Email: info@omkr.go.tz