Head image
Govt. Logo

Hits 115670 |  2 online

           


MAKAMU wa Kwanza wa Rais amesema, mapambano dhidi ya dawa za kulevya yanahitaji nguvu ya pamoja ili kuhakikisha nchi inashinda vita hivyo.
news phpto

MAKAMU wa Kwanza wa Rais, Othman Masoud Othman, amesema, mapambano dhidi ya dawa za kulevya yanahitaji nguvu ya pamoja ili kuhakikisha nchi inashinda vita hivyo.

MAKAMU wa Kwanza wa Rais, Othman Masoud Othman, amesema, mapambano dhidi ya dawa za kulevya yanahitaji nguvu ya pamoja ili kuhakikisha nchi inashinda vita hivyo.

Hayo aliyaeleza alipokuwa akifungua kongamano la wadau juu ya wajibu katika kupambana na dawa za kulevya nchini.

Alisema, mapambano hayo dhidi ya biashara na matumizi ya dawa za kulevya yanamuhusu kila mmoja wetu kwa vile athari zake humgusa kila mmoja wetu ndani ya jamii na taifa kwa ujumla.

Hivyo, alisema, jamii inapaswa kuongeza kasi ya kushirikiana katika kupambana na janga hilo kwa kuzingatia malengo yanayopangwa sambamba na kuhakikisha wimbi la uhalifu wa dawa za kulevya linasambaratishwa katika maeneo yote ya nchi.

Alisema, dawa za kulevya ni janga la kimataifa, na Zanzibanr ni miongoni mwa

nchi zilizoathiriwa na tatizo hilo, ambapo inakisiwa kuwa na takribani ya watu 10,000 wanaotumia dawa za kulevya, idadi hiyo sio ndogo na athari yake ni kubwa zaidi kuliko inavyofikiriwa.

Alisema, matumizi hayo yanachochea maradhi mbali mbali yakiwemo kensa, magonjwa ya akili, maambukizi ya UKIMWI maradhi ya homa ya Ini B – 8.4%, homa ya Ini C – 15.1% na mengine ya kujamiiana.

Alisema, hali hiyo inaonesha kwa jinsi gani nguvu kazi ya vijana inavyoweza kupotea kwa kasi na kuliacha taifa likipoteza nguvu kazi hiyo.

Alisema, kuna jumla ya kesi 654 katika mwaka 2018, kesi 503 kwa mwaka 2019 na kesi 454 kwa mwaka 2020, kwa mujibu wa taarifa za jeshi la polisi, hiyo ni ushahidi tosha kwamba dawa za kulevya zinaingizwa nchini.

Alisema, ili kufanikiwa katika kuyatekeleza mapambano hayo, ni wajibu wa kila mmoja kutoa mawazo yake juu ya mbinu bora zitakazosaidia kuleta matokeo chanya ikiwemo kuzifanyia kazi kesi za dawa za kulevya zinazochukua muda mrefu pasi na kupatiwa hatia.

Aidha, kuhakikisha wahusika wanachukuliwa hatua stahiki kwa mujibu wa sheria namba 9 ya mwaka 2009 na sheria nyengine zinazofanya kazi pamoja. "Endapo tukiyasimamia haya yote kwa uzalendo na kwa uadilifu mkubwa, tutaiwezesha serikali yetu kujenga uchumi imara na kufikia malengo tuliyojipangia".

Alisema, azma ya serikali ni kuona wananchi wake wanaishi katika maisha mazuri bila ya biashara wala matumizi ya dawa za kulevya na kuwaokoa vijana ili wawe warithi watakaokuja kuendeleza mipango, mikakati na malengo ya maendeleo ya nchi.

Hivyo, aliwataka wananchi kwa ujumla kuendelea kuwa wadau katika mapambano ya dawa za kulevya na siyo kuiachia taasisi au mtu mmoja hasa ikizingatiwa kwamba vita hivyo ni vikubwa na moja ya silaha zake ni mashirikiano ya pamoja.

Mkurugenzi Kinga, Tiba na Marekebisho ya Tabia, Tume ya Kitaifa ya Kuratibu, Kudhibiti Utumiaji Dawa za Kuelevya Zanzibar, Said Ramadhan Maulid, alisema, mafanikio kadhaa yamepatikana katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya nchi.

Alisema, bado zipo changamoto kadhaa ikiwemo uendeshaji wa kesi za dawa za kulevya na ushirikiano baina ya familia na hata vyombo vya ulinzi na usalama hautoshelezi.

"Sheria yetu ya udhibiti dawa za kulevya ipo vizuri, lakini, kuwa na sheria ni jambo moja na kuitekeleza ni jambo la pili".

"Tuna magari tumeyazuia yameungana na uhalifu 15, lakini, hadi sasa hakuna hatua inayoendelea, nyengine zinaharibika na kuoza haziisadia serikali wala wahusika".

Huduma za Tehama

Barua Pepe

Sisi

Mwanzo Kuhusu Sisi Idara Zetu

Viunga Muhimu

ZEMA ZAC DDA IKULU

Mawasiliano

Ofisi Kuu
S.L.P 2808, Migombani, Zanzibar
Tel.: +255(24)2232474 Mhe Waziri



Tel.: +255 (24)2232475 Katibu Mkuu,
Fax: +255 (24)2232476
Email: info@omkr.go.tz