Warning: session_start(): open(/var/cpanel/php/sessions/ea-php70/sess_fef7dd776a7ee34c60cce6e451f19e77, O_RDWR) failed: No space left on device (28) in /home/omkr/public_html/sess.php on line 17

Warning: session_start(): Failed to read session data: files (path: /var/cpanel/php/sessions/ea-php70) in /home/omkr/public_html/sess.php on line 17
fullview :: First Vice President office, Zanzibar
Head image
Govt. Logo

Hits 5476 |  2 online

           


TUZINGATIE HAKI ILI TUMALIZE UKIMWI_MHE. OTHMAN
news phpto

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, akiwa katika Kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani yaliyofanyika katika uwanja wa Gombani,Wilaya ya Chakechake,Mkoa wa Kusini Pemba; tarehe 01 Disemba 2024.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Othman Masoud Othman amesema suala la utoaji wa haki katika maeneo mbalimbali, ni chachu ya kupata matokeo makubwa, wakati huu ambao Dunia inapambana na Maradhi ya UKIMWI.

Ameyasema hayo, Disemba 01, 2024 wakati aliposhikiri akiwa Mgeni Rasmi katika Hafla ya Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani, huko Viwanja vya Gombani ya Kale, Wilaya ya Chake Chake, Mkoa wa Kusini Pemba.

Amesema maadhimisho ya Siku hio, ambayo yanafanyika Ulimwenguni kote, yanatoa fursa kwetu na kwa Nchi nyengine Duniani, kutafakari tuliyoyafanya katika kupambana na Janga hili, katika Kipindi kilichopita, na kujipanga upya, ili kukabiliana na changamoto zinazojitokeza, ambazo zinakwaza juhudi za kumaliza maambukizo mapya ifikapo Mwaka 2030, Mhe Othman ameyasema hayo, huku akiitaka jamii kujipanga kwa kulitokomeza Janga hilo.

Aidha, amesema Zanzibar imeweza kudhibiti Kiwango cha maambukizo ya Virusi vya UKIMWI, na kubaki chini ya Asilimia Moja (1%) ambapo Tafiti za hivi Karibuni zimeonyesha kuwa ni asilimia 0.4 ya Wakaazi wa Zanzibar, ambao wanaishi na Virusi vya UKIMWI.

Akitoa wasia na wito wake, kuhusu Mambo ya Msingi, ili kushinda Vita dhidi ya Janga Thakili la UKIMWI, Mheshimiwa Othman amesema, "ni wajibu kila mmoja wetu kuishi kwa tahadhari, kubadilisha tabia na kuwa na nyendo njema, pamoja na jamii kushikamana na utaratibu wa maadili na malezi jumuishi ya asili, ambao utaleta ujasiri, wa kuwakataza vijana na watoto, ambao ndio kwa kiasi kikubwa wapo pembezoni mwa dimbwi la hatari, ili wasitumbukie katika vishawishi vikiwemo vya ulevi, uasherati, dawa za kulevya na upofu wa mapenzi yasiyopevuka".

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Harusi Said Suleiman, ameonya kwamba Kilele cha Maadhimisho hayo, si jambo la kushangiria mno kwa raha na kujisahau, bali jukwaa la kutafakari juu ya Masaibu na Matatizo tele yanayotokana na Janga la UKIMWI Duniani, pamoja na namna ya kukabiliana nayo, au kulitokomeza kabisa.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mhe. Rashid Hadid Rashid, amefahamisha kuwa, licha ya Zanzibar kuendelea kubaki na Asilimia ndogo ya Maambukizi ya UKIMWI, bali Eneo lake limezungukwa na vichochezi vingi ambavyo ni hatari kwa rika zote za jamii, na hasa Vijana, ambao lazima walindwe na wachungwe sana, pamoja na wenyewe kuishi kwa tahadhari.

Akiwasilisha Taarifa ya Hali ya UKIMWI Nchini, Mwenyekiti wa Bodi ya Kamisheni ya UKIMWI Zanzibar, Bw. Ali Salim, akibainisha kwamba Rika Hatarishi dhidi ya Maambukizi Mapya ya UKIMWI, ni Watu wenye Umri wa Miaka 25 hadi 49, bali iwapo Jamii itazingatia, kwa umakini na upendo, upo uwezekano mkubwa wa kutokomeza changamoto zinazoletwa na Janga hilo.

Viongozi mbali mbali wa Serikali, Vyama vya Siasa, Wakurugenzi, Maafisa Wadhamini, Wadau wa mapambano dhidi ya UKIMWI, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Asasi za Kiraia, Wawakilishi wa Makampuni, Taasisi na Mashirika ya Kitaifa na Kimataifa, pamoja na Wananchi, wamehudhuria katika hafla hiyo, wakiongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hamza Hassan Juma; Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Bi Salama Mbarouk Khatib; Wakuu wa Wilaya zote Nne (4) za Pemba; Msimamizi Mkuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa Nchi, Bw. George Leroy; pamoja na Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Ndugu Ilyasa Pakacha Haji.

Huduma za Tehama

Barua Pepe

Sisi

Mwanzo Kuhusu Sisi Idara Zetu

Viunga Muhimu

ZEMA ZAC DDA IKULU

Mawasiliano

Ofisi Kuu
S.L.P 2808, Migombani, Zanzibar
Tel.: +255(24)2232474 Mhe Waziri



Tel.: +255 (24)2232475 Katibu Mkuu,
Fax: +255 (24)2232476
Email: info@omkr.go.tz