Head image
Govt. Logo

Hits 109922 |  5 online

           


Zanzibar Kupinga Matumizi ya Biashara Haramu ya Dawa za Kulevya
news phpto

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Mhe Masoud Ali Mohamed, amesema Serikali haitamvumilia mtu yeyote na kwa dhamana aliyonayo, atakaebainika kujihusisha na matumizi pamoja na usambazaji wa dawa za kulevya.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Mhe Masoud Ali Mohamed, amesema Serikali haitamvumilia mtu yeyote na kwa dhamana aliyonayo, atakaebainika kujihusisha na matumizi pamoja na usambazaji wa dawa za kulevya.

Akizungumza katika maadhimisho ya kupiga vita matumizi na usambazaji wa dàwa za kulevya katika uwanja wa Mapinduzi Square Kisonge, amesema dhamana ya uongozi ni kuwatumikia A

Mhe Masoud amevitaka vyombo vya ulinzi kutokuwa na muhali katika kuwafichua wanaojihusisha na biashara hiyo haramu, wakiwemo wafanyabiashara wasio waaminifu wanaojihusisha na biashara hiyo.

Nae Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Zanzibar, Kanal Zuberi Burhan Nassoro,amesema hadi sasa Mamlaka imekamata Jumla kesi 117 na kuzitaka mamlaka za sheria kuepuka vitendo vya rushwa ili kuweza kufanikisha vita hiyo.

Aidha amewaomba wazazi, walezi na viongozi wa dini kutumia nafasi zao kuuelimisha umma juu ya athari ya matumizi ya dawa za kulevya pia kuwapeleka vijana kwenye kituo cha Tiba, Kinga na Marekebisho ya Tabia, ambao kwa hiyari yao wameamua kuachana na matumizi ya Dawa za kulevya

Serikali kupitia Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya imeanzisha kituo cha Tiba, Kinga na Marekebisho ya Tabia, ili kuwanusuru vijana ambao wameathirika na Dawa za Kulevya, na kuwafundisha stadi za kazi, baada ya kupona ili wote walioathirika waweze kupata kazi za kufanya na kujikwamua kiuchumi

“Napenda kuchukua fursa hii kuwasihi wananchi kufichua wahalifu na wauzaji wa biashara haramu ya Dawa za Kulevya ni hekma na busara kila mtu kushiriki katika mapambano haya ili kunusuru, utamaduni, utu na silka ya mzanzibari” amesisitiza Kanal Burhani.

Akisoma risala ya waraibu waliopata nafuu, Msaidizi meneja kituo cha Tiba,Kinga na Marekebisho ya tabia cha Kidimni, Iddi Mussa Iddi, amesema katika mafanikio Jumla ya vijana elfu nne wameshapata nafuu Zanzibar, na kwa sasa Vijana 32 wanaendelea na Tiba katika nyumba hiyo.

Akitoa salamu za Mkoa, Mkuu wa Mkoa Mjini Magharib Mhe Idrissa Kitwana Mustafa, amesema hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi ya Sheha wa Shehiya atakaeshindwa kutoa ushirikiano kwa Mamlaka hiyo katika vita ya kupambana na dawa za kulevya.

Kila ifikapo tarehe 26 Juni ya kila mwaka Dunia huadhimisha kupinga matumizi ya biashara haramu ya Dawa za Kulevya, iliyopitishwa katika kikao cha Baraza la Umoja wa Mataifa mwaka 1987, Ujumbe wa mwaka huu ni Kukabiliana na Changamoto ya dawa za kulevya katika masuala ya kiafya na majanga ya kibinaadamu

Huduma za Tehama

Barua Pepe

Sisi

Mwanzo Kuhusu Sisi Idara Zetu

Viunga Muhimu

ZEMA ZAC DDA IKULU

Mawasiliano

Ofisi Kuu
S.L.P 2808, Migombani, Zanzibar
Tel.: +255(24)2232474 Mhe Waziri



Tel.: +255 (24)2232475 Katibu Mkuu,
Fax: +255 (24)2232476
Email: info@omkr.go.tz