Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe Harusi Said Suleiman ametaka wafanyakazi wa Taasisi zilizo chini yake kuunga mkono jitihada za Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi katika kutekeza majukumu yao ya kiutendaji
Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe Harusi Said Suleiman ametaka wafanyakazi wa Taasisi zilizo chini yake kuunga mkono jitihada za Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi katika kutekeza majukumu yao ya kiutendaji
Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wafanyakazi kwa nyakati tofauti wa Tume ya UKIMWI Baraza la Taifa la Watu wenye Ulemavu ambapo amesisitiza suala la nidhamu na uadilifu katika utendaji wao wa kazi na kuwa na mashirikiano ya pamoja ili waweze kujitathmini vyema na kujipima utendaji wao wa kazi
Mhe Harusi amesema kuwa haipendezi kuona wafanyakazi wanabaki ofisini badala yake waende kwa jamii kuwatumikia kwa kutoa elimu hasa skuli, vyuo vikuu na madrasa kwani vishawishi vingi huanzia huko na matokeo yake watoto wadogo wanajiingiza kwenye matendo maovu yakiwemo ya zinaa hatimae kuwepelekea maambukizi ya UKIMWI
“Makosa yakitokezea yanakwenda Serikalini zidisheni juhudi ya mapambano dhidi ya UKIMWI watoto wadogo wanaathirika tu, Taifa hili linatuamini nasi tujiaminishe” alisisitiza Mhe Harusi
Aidha ameagiza kufanyika kwa tathmini ili kufahamu hali halisi ya maradhi ya UKIMWI na kujipanga vyema kuona kipi kinakosekana katika utowaji waelimu ili asilimia iliyopo ya 0.4 isije ikaongezeka na kurudisha nyuma maendeleo na jitihada zilizokwisha kufanyika katika kipindi chote tokea kuingia na kugundulika kwa maradhi ya UKIMWI hapa Zanzibar
Kwa Upande wa Baraza la Taifa la Watu wenye Ulemavu amewataka wafanyakazi wote kufanya kwa mashirikiano bila kujali nani anaulemavu na nani hana na kuisaidia Serikali katika kupanga mipango yake ya maendeleo kwa maendeleo jumuishi
Kwa upande wao wakurugenzi wa Taasisi hizo Mkurugenzi Mtendaji Tume ya UKIMWI Dkt Ahmeid M. Khatib Reja amemuelezea Waziri Harusi kuwa moja kati ya mikakati ya Tume ni kuhakikisha wanaendelea kuyafikia makundi maalum ambayo ndio hatarishi yakiwemo wana