Head image
Govt. Logo

Hits 111488 |  4 online

           


TUNATHAMINI JUHUDI ZA WATU WA CHINA KATIKA KUSAIDIA MAENDELEO ZANZIBAR- MHE. OTHMAN
news phpto

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inathamini juhudi za Jamhuri ya Watu wa China katika kuhamasisha maendeleo na ujenzi wa ustawi wa jamii na Nchi kwa ujumla.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inathamini juhudi za Jamhuri ya Watu wa China katika kuhamasisha maendeleo na ujenzi wa ustawi wa jamii na Nchi kwa ujumla.

Mheshimiwa Othman ameyasema hayo leo katika mazungumzo yake na Balozi wa China nchini Tanzania, Bibi Chen Ming Jian, uliomtembelea Ofisini kwake Migombani, Jijini hapa kwa lengo la kukabidhi Msaada wa Visaidizi kwaajili ya watu wenye Ulemavu.

Amesema Serikali inatambua kwamba Jamhuri ya Watu wa China imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia maendeleo ya sekta mbali mbali hapa visiwani zikiwemo za afya na elimu.

Mheshimiwa Othman ameeleza kuwa ni wajibu wa kila upande kati ya Jamhuri mbili hizi zenye mashirikiano na fungamano la tokea enzi, na hivyo hapana budi kuongeza mahusiano kwa kufungua milango zaidi ya kusaidiana.

“Tunachukua nafasi hii kuwashukuru kwa dhati kabisa ndugu zetu wa Jamhuri ya Watu wa China kwa misaada na mashirikiano wanayoyatekeleza kwa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla na hivyo ni wajibu wetu kuyaendeleza mahusiano haya kwa kadiri itakavyowezekana”, amesema Mheshimiwa Othman.

Aidha Mheshimiwa Othman ameahidi kuwa Serikali ya Awamu ya Nane itaendelea kufungua milango katika kukuza mashirikiano yatakayoweka mazingira bora ya kusaidiana kati ya pande mbili hizo.

Mheshimiwa Othman ameshuhudia hafla ya uwekaji saini makabidhiano ya visaidizi hivyo kwa watu wenye ulemavu, kutoka kwa Ubalozi wa China nchini, kupitia Mradi wa Rafiki (Rafiki Program), msaada ambao umejumuisha pia viti na fimbo nyeupe, vyenye thamani ya takriban Shilingi za Kitanzania 59 Milioni.

Akikabidhi msaada huo, Balozi wa China nchini Tanzania, Bibi Chen Ming Jian ameeleza kuwa, pamoja na urafiki wa muda mrefu kati ya Zanzibar na Nchi yake, wamechukua hatua hiyo kwa kuthamini pia maisha na ustawi wa watu wa visiwa hivi, hasa wenye ulemavu.

Balozi huyo amesifia na kushukuru juhudi za kuendeleza mahusiano mema kati ya Jamhuri ya Watu wa China na Zanzibar, huku akiahidi kutosita kufanikisha misaada ya hali na mali kwa Zanzibar na kwa kadiri itakavyowezekana.

Hafla hiyo imewajumuisha pia viongozi mbali mbali, ambao ni pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Harusi Said Suleiman, Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Dokta Omar Dadi Shajak na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira, Bw. Sheha Mjaja Juma.

Huduma za Tehama

Barua Pepe

Sisi

Mwanzo Kuhusu Sisi Idara Zetu

Viunga Muhimu

ZEMA ZAC DDA IKULU

Mawasiliano

Ofisi Kuu
S.L.P 2808, Migombani, Zanzibar
Tel.: +255(24)2232474 Mhe Waziri



Tel.: +255 (24)2232475 Katibu Mkuu,
Fax: +255 (24)2232476
Email: info@omkr.go.tz