Head image
Govt. Logo

Hits 110847 |  3 online

           


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar amesema UKIMWI upo na ni tishio kwa ustawi wa maisha ya watu na maendeleo ya nchi.
news phpto

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe Othman Masoud Othman amesema licha ya mafanikio yaliyofikiwa katika juhudi za kupambana na UKIMWI, lakini bado unaendelea kuwa tishio kwa ustawi wa maisha ya watu na maendeleo ya nchi.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe Othman Masoud Othman amesema licha ya mafanikio yaliyofikiwa katika juhudi za kupambana na UKIMWI, lakini bado unaendelea kuwa tishio kwa ustawi wa maisha ya watu na maendeleo ya nchi.

Mheshimiwa Othman ameyasema hayo leo katika hafla ya kilele cha maadhimisho ya Kitaifa Siku ya UKIMWI Duniani, yaliyofanyika Wilaya ya Kati, Shehia ya Ubago, Mkoa wa Kusini Unguja.

Amesema kuwa ingawa Zanzibar imefanikiwa kwa kiwango kikubwa kufikia malengo ya kudhibiti UKIMWI, ikiwemo kiwango cha chini ya asilimia moja (1%) ya maambukizi hapa visiwani, uchambuzi wa takwimu mbali mbali unaonyesha kwamba bado kuna baadhi ya makundi hayajaweza kufikiwa ipasavyo na huduma zinazotolewa.

Mheshimiwa Othman amebainisha kuwa wanawake katika visiwa vya Unguja na Pemba wanaonekana kufanya vyema katika kuzifikia na kuzitumia huduma zikiwemo za ushauri nasaha, upimaji wa Virusi vya UKIMWI (VVU) na kuvipunguza mwilini, na pia matumizi ya dawa za kupunguza makali ya virusi (ARV).

Akifafanua baadhi ya takwimu, Mheshimiwa Othman amesema, “katika watu 166,566 waliopatiwa huduma za ushauri nasaha na uchunguzi wa VVU kati ya Januari hadi Septemba mwaka huu hapa Zanzibar, wengi wao walikuwa ni wanawake ambao ni idadi ya 86,947 ukilinganisha na 79,619 idadi ya wanaume, aidha kati ya watu 7,481 wanaotumia dawa za ARVs hadi kufikia Septemba mwaka huu, 5,170 ni wanawake ukilinganisha na idadi ya wanaume 2,427 ambapo tofauti hizi zina athari kubwa katika kudhibiti maambukizi ya VVU na kulimaliza janga la UKIMWI”.

Akieleza changamoto mbali mbali katika kukabiliana na maabukizi ya UKIMWI, zikiwemo za unyanyapaa na kushindwa kujielewa kwa baadhi ya makundi-athirika, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Dkt Saada Mkuya Salum, amesema kuwa kupitia Tume ya UKIMWI Zanzibar, Serikali itahakikisha inaandaa mbinu mbadala ili ifikapo mwaka 2030, yasiwepo maambukizi mapya hapa katika Visiwa hivi.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Bw. Hadidi Rashid Hadidi, amesema kuwa hadi kufikia maadhimisho ya mwaka huu, bado idadi ya maambukizi ya UKIMWI katika Mkoa wake inabaki kuwa kubwa, kulinganisha na mikoa mingine ya Zanzibar, kutokana na kukithiri kwa nyumba zinauzwa ulevi, uwepo wa baa nyingi, kumbi za starehe ambazo ndio chanzo cha kufanyika kwa matendo yanayopelekea ngono zembe.

Harakati za maadhimisho ya siku hii hulenga zaidi katika kuongeza uelewa kwa jamii juu ya maradhi ya UKIMWI, kuishajihisha jamii kujiepusha na mambo ambayo yanachangia maambukizo ya VVU, kueleza mafanikio, changamoto na mikakati itakayosaidia katika kudhibiti maambukizi ya VVU, kuwafariji, kuonyesha mshikamano kwa watu wanaoishi na Virusi Vya UKIMWI, na kuwakumbuka wale waliopoteza maisha yao kutokana na maradhi ya UKIMWI.

Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani , huadhimishwa kila ifikapo Disemba 1, ambapo mwaka huu 2021 yamechukua kauli mbiu inayosema “TUWEKE USAWA KUMALIZA UKIMWI NA MAJANGA MENGINE”, ikiwa ni msisitizo katika kuweka usawa wa upatikanaji wa huduma za kinga na tiba kwa watu wote.

Viongozi mbali mbali wa Serikali na Kijamii, Mashirika ya Kitaifa na Kimataifa, Washirika wa Maendeleo na Asasi za Kiraia, wamejumuika katika maadhimisho hayo, akiwemo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe Khamis Hamza Chilo (Mb), Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Dkt. Omar D. Shajak, Mkuu wa Wilaya ya Kati Unguja, Bi Marina Joel Thomas na Mwakilishi kutoka Umoja wa Mataifa (UN), Dr. George Loy. 

Huduma za Tehama

Barua Pepe

Sisi

Mwanzo Kuhusu Sisi Idara Zetu

Viunga Muhimu

ZEMA ZAC DDA IKULU

Mawasiliano

Ofisi Kuu
S.L.P 2808, Migombani, Zanzibar
Tel.: +255(24)2232474 Mhe Waziri



Tel.: +255 (24)2232475 Katibu Mkuu,
Fax: +255 (24)2232476
Email: info@omkr.go.tz