Head image
Govt. Logo

Hits 110589 |  4 online

           


Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais amelishukuru shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani UNFPA kwa juhudi inazozichukuwa katika kusaidia Watu wenye Ulemavu
news phpto

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Dkt Omar.D Shajak amelishukuru shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani UNFPA kwa juhudi inazozichukuwa katika kusaidia Watu wenye Ulemavu

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Dkt Omar.D Shajak amelishukuru shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani UNFPA kwa juhudi inazozichukuwa katika kusaidia Watu wenye Ulemavu

Ameeleza hayo ofisini kwake Migombani alipofanya mazungumzo na Msaidizi Mwakilishi mkaazi wa UNFPA Dkt Wilfred Ochan kuhusiana na nafasi ya Watu wenye Ulemavu katika maendeleo ya nchi na kutoa shukurani kwa shirika hilo kwa kusaidia kuanzisha mfumo jumuishi wa Watu wenye Ulemavu

Dkt Shajak amesema kuwepo kwa mfumo jumuishi wa Watu wenye Ulemavu umekuwa ni suluhisho katika kuisaidia Serikali kufanya maamuzi sahihi kwa vile unawezesha kujua idadi ya Watu wenye Ulemavu, aina ya ulemavu wao na kiwango chake pamoja na mahitaji yao

Amesema mfumo jumuishi unaweka takwimu sahihi kufahamu ukubwa na udogo wa mahitaji ya Watu wenye Ulemavu na hatimae serikali kufanya maamuzi mazuri katika ya utekelezaji wa mipango yake kuanzia ngazi ya shehia hadi serikali kuu

Aidha amesema pamoja na kuwepo kwa mfumo huo lakini bado unahitaji maboresho ili uweze kwenda mbali hivyo kupitia UNFPA anaimani wataweza kufikia malengo na watu wenye Ulemavu kupata stahiki zao zote ikiwemo kuwajengea uwezo kielimu, afya na ushiriki wao katika masuala ya maendeleo ya kiuchumi

Nae Msaidizi Mwakilishi mkaazi wa UNFPA Dkt Wilfred Ochan amesifu jitihada zinazochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais kwa juhudi wanazozichukuwa katika kuwasaidia Watu Wenye Ulemavu

Amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha masuala ya Watu wenye Ulemavu yanaendelea kutambuliwa na kuingizwa katika sera kwenye sekta mbali mbali kama vile afya, elimu, miundombinu shirikishi, makaazi na ajira ilikuwepo na ufanisi

Kupitia UNFPA wameahidi kuendelea kufanya kazi na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais kupitia Baraza la Watu wenye Ulemavu na kuona namna ya kufanya mashauriano katika mpango mkuu wa miaka mitano ujao ili kuyaingiza masuala ya Watu wenye Ulemavu yakiwemo masuala ya afya ya uzazi na kuwajengea uwezo kielimu

Huduma za Tehama

Barua Pepe

Sisi

Mwanzo Kuhusu Sisi Idara Zetu

Viunga Muhimu

ZEMA ZAC DDA IKULU

Mawasiliano

Ofisi Kuu
S.L.P 2808, Migombani, Zanzibar
Tel.: +255(24)2232474 Mhe Waziri



Tel.: +255 (24)2232475 Katibu Mkuu,
Fax: +255 (24)2232476
Email: info@omkr.go.tz