Head image
Govt. Logo

Hits 110213 |  4 online

           


Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais Dkt Omar D Shajak amemkabidhi kiti cha magurudumu mawili chenye kutumia chaji (motor wheel chair)
news phpto

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais Dkt Omar D Shajak amemkabidhi kiti cha magurudumu mawili chenye kutumia chaji (motor wheel chair) Bi Zahra Waziri Said wa Skuli ya Sayansi na Tiba Mbweni Chuo kikuu cha Suza anaechukuwa Stashahada ya Famasia mwaka wa pili.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais Dkt Omar D Shajak amemkabidhi kiti cha magurudumu mawili chenye kutumia chaji (motor wheel chair) Bi Zahra Waziri Said wa Skuli ya Sayansi na Tiba Mbweni Chuo kikuu cha Suza anaechukuwa Stashahada ya Famasia mwaka wa pili.

Akimkabidhi kiti kisaidizi hicho Dkt Shajak amesema kuwa kitamsaidia Zahra katika shughuli zake za masomo na kurahisisha majukumu yake mengine kiutendaji pamoja harakati zake za kwenda na kurudi chuoni na kwengineko.

Dkt Shajak amefarijika na uwezo wa Zahra na kusema kuwa ni mfano mzuri wa kuigwa kwani kila binaadamu anauwezo wake hivyo Ulemavu wake sio sababu ya kumfanya mtu kukosa fursa muhimu za amali

“huu ni mfano mwema na kigezo kizuri cha wengine waweze kuiga mfano wako na kujuwa kuwa Mwenyezi Mungu akikupa ulemavu wowote sio kama umekosa fursa nyengine kwani Watu wenye ulemavu wakirahisishiwa mazingira yao wanafanya vizuri zaidi”

Katibu Shajak amesema Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais kupitia Baraza la Watu wenye Ulemavu itaendelea kuratibu na kusaidia Watu wenye Ulemavu waweze kusoma katika mazingira mepesi na wale wanaofanya kazi pia na wao wafanye kazi zao katika mazingira rafiki

Nae Zahra Waziri Saidi ameishukuru Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais kupitia Baraza la Taifa la Watu wenye Ulemavu kwa kumpatia kiti kisaidizi hicho “MotorWheelchair” ambacho aliihitaji kwa muda mrefu sana na kuahidi atakitunza vyema.

Aidha amewashukuru wale wote waliojitahidi na kuhakikisha anapata kiti kisaidizi kwa ili kurahisisha majukumu yake ya masomo na harakati za kujiendeleza

Mkurugenzi Baraza la Taifa la Watu wenye Ulemavu Inginia Ussy Khamis Debe kupitia Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais amesema Baraza litahakikisha kwamba Watu wenye Ulemavu wanapata fursa sawa za elimu, afya na Mambo mengine ya kijamii hasa ya kujiendesha kimaisha.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inadhamira njema kwa wananchi wake wote na imeweka mazingatio kwa Watu wenye Ulemavu kuona wanapata fursa sawa ya kielimu na fursa nyengine za kijamii ukiwemo uwezeshaji na Miundo mbinu Rafiki ili waweze kujimarisha kiuchumi.

Kiti kisaidizi kimetolewa na Baraza la Taifa la Watu wenye Ulemavu kina thamani ya shilingi za Kitanzania Milion tatu ambapo makabidhiano hayo yamefanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Makamu wa Rais Migombani, Mjini Zanzibar

Huduma za Tehama

Barua Pepe

Sisi

Mwanzo Kuhusu Sisi Idara Zetu

Viunga Muhimu

ZEMA ZAC DDA IKULU

Mawasiliano

Ofisi Kuu
S.L.P 2808, Migombani, Zanzibar
Tel.: +255(24)2232474 Mhe Waziri



Tel.: +255 (24)2232475 Katibu Mkuu,
Fax: +255 (24)2232476
Email: info@omkr.go.tz