Ofisi ya Faragha ya Makamu wa Kwanza wa Rais
Madhumuni
Ofisi ya Faragha ya Makamu wa Kwanza wa Rais inafanya kazi za kuratibu shughuli zote za Mheshimiwa Makamu wa Kwanza wa Rais na kutoa huduma zote muhimu kwa Mheshimiwa Makamu wa Kwanza wa Rais na familia yake pamoja na kutunza makaazi ya Makamu wa Kwanza wa Rais yaliyoko Mazizini Unguja. Majukumu mengine ya Ofisi ya Faragha ni kama yafuatayo:-
Kazi za Ofisi
- Kuwa ni msingi wa mawasiliano baina ya Mheshimiwa Makamu wa Kwanza wa Rais na Serikali hasa viongozi na wananchi.;
- Kumsaidia Mheshimiwa Makamu wa Kwanza wa Rais katika masuala yote ya kuimarisha mahusiano na jamii.;
- Kutunza makaazi ya Mheshimiwa Makamu wa Kwanza wa Rais yaliyoko Mazizini Unguja.;
- Kufanya tafiti kutambua na kuchunguza maeneo yenye udhaifu katika ufikishwaji wa huduma za haki, kutayarisha na kutekeleza mbinu za kupunguza/kuondosha malalamiko hayo;
- Kuratibu na kufuatilia utekelezaji wa ahadi za Mheshimiwa Makamu wa Rais alizozitoa kwa wananchi.;
- Kuimarisha mashirikiano na mahusiano ya Kitaifa na Kimataifa kwa kukutana na Mabalozi na Wageni Mashuhur; na
- Kuratibu ziara za Mheshimiwa Makamu wa Kwanza za ndani na nje ya nchi.